Na Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mwaka huu, mvutano kati ya Simba SC na Yanga SC umeongezeka kutokana na sababu mbalimbali za kiutawala, kikanuni, na kihistoria, ambazo zimeathiri ratiba na uchezaji wa mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu iliyopangwa kufanyika Machi 8, 2025, iliahirishwa baada ya Simba kugomea kucheza kwa madai ya kunyimwa haki ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa siku moja kabla ya mechi, kama inavyotakiwa na Kanuni ya 17(45) ya Ligi Kuu. TPLB ilithibitisha kuwa Simba hawakuwasiliana rasmi na mamlaka za uwanja kuhusu nia yao ya kufanya mazoezi, hivyo kusababisha sintofahamu na kuahirishwa kwa mechi hiyo .
Licha ya mvutano uliopo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuwa mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga na Simba itachezwa Juni 15, 2025, saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Hata hivyo, Yanga bado wameshikilia msimamo wao wa kutoshiriki mechi hiyo, wakieleza kuwa hawana imani na vyombo vya maamuzi vya ndani vya soka .
Siku chache zilizopita katika mchezo wa NBC premier league Simba iliibuka na ushindi wa bao Moja kwa bila dhidi ya Singida lakini maswali yamezidi kuwa mengi kwanini Simba apoteze kwa idadi kubwa ya magoli ilihali angeshinda angeweza kukutan na Yanga katika fainal ya CRDB federation,kingine kinacho onyesha Simba waliokuwa wanakimbia derby ni kutokana kutoanzishwa kwa wachezaji muhimu kwenye mchezo huo mchezaji kama Elie Mpanzu, Muhammed Hussein na Shomari kapombe walianzia benchi.
0757915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment