Timothy Lugembe
Mwanakwetusports.
Beki mahiri kutoka Uruguay, Ronald Araújo, hatimaye amevunja ukimya juu ya tetesi zinazomhusisha na kuondoka klabu ya Barcelona.
Katika taarifa aliyopost kupitia mitandao ya kijamii, Araújo ameweka bayana kuwa bado ni sehemu ya kikosi cha Barcelona na kwamba hana mpango wa kuondoka. Hii ni baada ya kuwepo kwa uvumi mwingi ulioenea kwenye vyombo vya habari na mitandao kuhusu mustakabali wake.
Kwa kutumia ujumbe mfupi lakini wenye uzito, Araújo alithibitisha kuwa anajivunia kuwa mchezaji wa Barcelona na ataendelea kupambana kwa ajili ya timu hiyo. “Sitoki,” aliandika kwa kifupi, akihitimisha kwa emoji zinazoashiria uthabiti na mapenzi kwa klabu.
Ujumbe huu umewatuliza mashabiki wa Barcelona ambao walikuwa na hofu ya kumpoteza mmoja wa mabeki bora waliopo sasa, huku klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zikihusishwa na nia ya kumsajili.
Kwa ujumbe huo, inaonekana Araújo bado ana ndoto ya kuendelea kulitumikia taifa la Catalonia kupitia klabu ya Barcelona, akilenga mafanikio zaidi katika misimu ijayo.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment