RAUNDI YA 16 IPO TAYARI, NUNO MENDES ATAWEZA KUMZUIA LIONEL MESSI?

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain (PSG), Nuno Mendes, ameendelea kuvutia macho ya mashabiki na wachambuzi wa soka baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mechi kadhaa za FIFA Club World Cup msimu wa 2024/2025.

Katika hatua ya awali, Mendes aliwazima mastaa wakubwa kama Mohamed Salah (Liverpool), Bukayo Saka (Arsenal), na kijana hatari kutoka Barcelona, Lamine Yamal. Sasa macho yote yameelekezwa kwenye mechi inayofuata ambapo PSG watavaana na Inter Miami ya Lionel Messi katika hatua ya 16 bora .

Macho na masikio ya Mashabiki wa soka duniani yapo siku ya June 29 wakiwa wanasubiri kwa hamu kuona kama Mendes ataweza kuzuia maarifa ya mshindi huyo mara nane wa Ballon d'Or, ambaye kwa sasa anakipiga katika ligi ya Marekani (MLS) kupitia klabu ya Inter Miami.

Mbali na mchezo huo katika hatua ya 16 Bora pia Kuna michezo mingine ambapo June 28 Kuna michezo miwili SE Palmeiras vs Botafogo , SL Benfica vs Chelsea, June 29 itakuwa ni PSG vs Inter Miami, Flamengo vs Bayern Munich, June 30 itakuwa ni Inter Milano vs Fluminense, huku Julai 1 ikiwa ni Man City vs Al Hilal, Real Madrid vs Juventus, huku mchezo wa mwisho ukiwa ni Julai 2 Dortmund vs Monterrey.

Je ? nani kukata tiketi ya kusonga mbele hatua inayo fuata majibu tutayapata, na je? Nuno mendes atafanikiwa kuzuia uwezo wa Messi uwanjani Kila kitu kitakuwa Waziri baada ya michezo hiyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments