Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ratiba rasmi ya Ligi Kuu ya England (Premier League) kwa msimu wa 2025/2026 imetangazwa leo Juni 18, ikionesha mfululizo wa mechi 380 zitakazochezwa kuanzia Ijumaa, Agosti 15 hadi Jumapili, Mei 24, 2026.
Mabingwa watetezi Liverpool watafungua msimu kwa kuikaribisha Bournemouth katika uwanja wa Anfield siku ya Ijumaa Agosti 15, Mechi hiyo itaashiria mwanzo wa msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi.
Katika mechi kubwa ya ufunguzi wa Jumapili Agosti 17, Manchester United watawakaribisha Arsenal katika dimba la Old Trafford kwenye kile kinachoitwa “Super Sunday”. Hii ni moja ya mechi zinazotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi duniani.
Kwa upande mwingine, timu mpya zilizopanda daraja Leeds United, Burnley na Sunderland zitapambana kuonesha ubora wao kwenye ligi kuu. Sunderland, waliorejea ligi kuu baada ya miaka kadhaa, watafungua msimu nyumbani dhidi ya West Ham United.
Ligi Kuu ya England pia imethibitisha kuwa hakutakuwa na mechi siku ya Krismasi na kila timu itapewa mapumziko ya angalau saa 48 kati ya mechi husika, hasa kipindi cha sikukuu, Msimu huu pia utashuhudia matumizi ya teknolojia mpya ya kusaidia kuamua offside kwa haraka (semi-automated offside technology), pamoja na mpira mpya utakaotolewa na kampuni ya Puma.
Mashabiki wa soka wanatarajia msimu wa kusisimua, ukiwa na michezo mikubwa ya awali na derbi zinazotarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment