Timothy Lugembe,
Mwanakwetu sports.
Baada ya mgogoro wa muda mrefu kuhusu mchezo wa derby ya kariakoo kati ya simba na yanga kuwa na sintofahamu hatimaye makubaliano ya pamoja yamepatikana chini ya ushawishi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kikao cha tarehe 13 june 2025.
Rais Samia Suluhu alishiriki kikao na viongozi wa timu zote mbili pamoja na viongozi wa TFF na Bodi ya ligi, kikao hicho kili lenga kutafuta suluhisho juu ya mustakabali mzima wa soka la Tanzania baada ya timu ya Yanga kugomea mchezo wa june 15, 2025 kikao hicho kilienda vizuri na muafaka ulifikiwa kwa tarehe ya derby kupangwa upya na sasa mchezo huo utafanyika tarehe 25 june 2025 uwanja wa Benjamini Mkapa majira ya saa 11:00 jioni.
Baada ya uamuzi huo hakuna timu iliyo pinga maamuzi na kinachosubiriwa na maandalizi ya mchezo huo, ambapo kila timu imebakiza michezo miwili mpaka siku ya derby ambapo iwapo kila timu ikishinda michezo yake miwili , mchezo wa derby unatarajiwa kuwa mgumu kwani simba atahitaji kushinda mchezo ili awe bingwa huku Yanga atahitajika kushinda au kusare ili achukue ubingwa.
0767915473,
Lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment