Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Pyramids FC ya Misri imetwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya kuifunga Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2.
Mchezo wa kwanza ulivo fanyika nchini Africa kusini Pretoria, Mei 24, 2025 Mamelodi Sundowns 1 - 1 Pyramids , Mchezo wa pili uliofanyika nchini misri Cairo, Juni 1, 2025 Pyramids FC 2 - 1 Mamelodi Sundowns, Jumla ya mabao: Pyramids FC 3 - 2 Mamelodi Sundowns
Katika fainali hiyo ya mkondo wa pili magoli yalifungwa mnamo dakika ya 23': Fiston Mayele aliifungia Pyramids bao la kwanza baada ya kosa la ulinzi wa Sundowns, na dakika ya 56': Ahmed Samy aliongeza bao la pili kwa kichwa kutoka kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mohamed Chibi, na dakika ya 75' Iqraam Rayners alipunguza tofauti kwa Sundowns kwa shuti la volley kutoka ndani ya boksi na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Pyramids walidhibiti mchezo hadi mwisho licha ya presha kubwa kutoka kwa Mamelod hivyo kufanikisha ushindi wa kihistoria kwa kutwaa ubingwa wao kwa mara ya kwanza kutoka kuanzishwa kwake mwaka 2008 kwa Jumla ya USHINDI wa bao 3-2.
Timu ya pyramid imepata mafanikio makubwa msimu huu ikiwemo kumaliza nafasi ya pili katika liguu ya misri na hiyo imetokana na sintofahamu iliyotokea katika ligi hiyo ambapo ilitarajiwa Ahaly wangekatwa alama tatu kutokana na kutoka shiriki mchezo wao na zamaleck lakini haikuwa hivyo pia wamefanikiwa kutoa mfungaji Bora wa mashindano ya klabu bingwa fiston mayele mwenye magoli sita na wametwaa taji la klabu bingwa Africa.
Mafanikio haya yote ni matokeo mazuri ya uwekezaji ambao ulianza rasmi mwaka 2008 na mwaka 2018, klabu ilinunuliwa na Turki Al-Sheikh, bilionea kutoka Saudi Arabia na mshauri wa michezo wa kifalme.Baada ya kuinunua, aliibadilisha jina kutoka Al Assiouty kuwa Pyramids FCAlihamisha makao ya klabu kwenda Cairo na kuwekeza mamilioni ya dola kuijenga upya.na matunda yake yameanza kuonekana hivi sasa.
0767915471,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment