Na Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports,
TIMU YA PSG imetwaa ubingwa wa UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika historia yake, baada ya kuichapa Inter Milan ya nchini Italy kwa jumla ya mabao 5-0 katika fainali iliyochezwa uwanja wa Allianz Arena, Munich tarehe 31 Mei 2025.
Katika historia ya UEFA hakuna timu iliwahi kushinda kwa USHINDI mkubwa kama walio upata PSG huko Allianz arena Ushindi huu wa 5-0 ni ushindi mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika fainali ya Champions League tangu kuanzishwa kwa mashindano haya mwaka 1956, katika mchezo huo magoli yalifungwa na Achraf Hakim dakika ya 12, Desire Doue dakika ya 20 na 64, Khivicha Kvaratskheria 73 na msumari wa mwisho ulipigiliwa na Senny Mayulu dakika 86.
Désiré Doué miaka 19 , alifunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao moja, akawa mchezaji wa tatu kijana zaidi kuwahi kufunga katika fainali ya Champions League, akijiunga na Patrick Kluivert na Carlos Alberto, Kocha Luis Enrique alishinda fainali yake ya 11 ya klabu, akiendeleza rekodi yake ya kushinda kila fainali aliyofikia.
PSG imekamilisha msimu kwa kutwaa mataji matatu (treble) yaani Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Kombe la Ufaransa (Coupe de France), na sasa Ligi ya Mabingwa Ulaya( UEFA CHAMPIONS LEAGUE), Haya ni mafanikio makubwa zaidi ambayo PSG wameweza kuyapata toka kuanzishwa kwake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment