Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Athletic Club, Nico Williams, ameripotiwa kuwa na nia kubwa ya kujiunga na klabu ya FC Barcelona msimu ujao, licha ya kuwaniwa na vilabu vikubwa barani Ulaya kama Bayern Munich, na Arsenal.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya michezo barani Ulaya, Nico ameweka wazi kuwa Barcelona ndiyo chaguo lake la kwanza, Mchezaji huyo amekuwa katika kiwango bora akiwa na Athletic Bilbao, anaripotiwa kuwa tayari hata kupunguza mshahara wake ili kufanikisha ndoto yake ya kuvalia jezi ya Barcelona.
Barcelona, chini ya kocha Hansi Flick, imeonyesha nia ya dhati ya kumsajili kinda huyo ambaye pia amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania, Ripoti zinaeleza kuwa klabu hiyo iko tayari kuanza mazungumzo rasmi na Athletic Bilbao kuhusu kifungu cha kuvunja mkataba wa Nico ambacho kinakadiriwa kuwa kati ya euro milioni 58 hadi 62.
Hata hivyo, bado kuna mashaka ndani ya uongozi wa Barca, hasa kutoka kwa Rais Joan Laporta ambaye inasemekana kuwa na hofu juu ya uwezekano wa usajili huo, Pia inaripotiwa kuwa Barcelona bado inamvutiwa na mshambuliaji wa Liverpool, Luis Díaz, kama mbadala wa Nico.
Iwapo dili hili litatimia, Nico Williams atakuwa miongoni mwa vijana wa kisasa wenye kipaji kikubwa wanaojiunga na kikosi cha Barcelona kilichojaa vipaji kama Lamine Yamal, Pedri na Gavi, huku akitarajiwa kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment