Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imeendelea siku ya June 18, 2025, kwa kushuhudia Miamba ya soka nchini Simba na Yanga wakitoa vichapo kwa wapinzani wao kwa Kila timu kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 na kuzifanya mbio za ubingwa kuzidi kuwa ngumu na za kuvutia.
Simba SC wakicheza ugenini katika Uwanja Ali Hassan Mwinyi Tabora waliikandamiza KenGold FC kwa mabao 5-0 katika mchezo uliotawaliwa na kasi, ubunifu na nidhamu ya hali ya juu, Denis Kibu alikuwa moto wa kuotea mbali akiifungia Simba mabao mawili, huku Elie Mpanzu na Leonel Ateba wakiongeza msukumo kwa kuchangia mabao mengine.
Katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Yanga SC waliendeleza ubabe wao kwa kuichapa Tanzania Prisons mabao 5-0, katika mchezo uliokuwa wa upande mmoja kwa muda mwingi. Wachezaji walio ng'ara ni pamoja na Mudathir Yahya, Clatous Chama, Pacome Zouzoua, na Israel Mwend, kwa kupachika mabao huku mchezaji nyota akiwa Pacome zouzoua.
Yanga SC kwa sasa wanaongoza ligi kwa alama 76 baada ya michezo 28, na ushindi huo umeimarisha nafasi yao ya kutetea taji walilotwaa msimu uliopita huku Simba nao wamefikisha alama 75 baada ya mechi 28, wakisalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi lakini wakiwa nyuma kwa alama moja tu dhidi ya vinara Yanga SC huku Kila timu ikiwa imebakiza michezo miwili mmoja ni baina Yao siku ya June 25 mwaka huu.
Maswali ni je? Simba ataendelea kuonyesha unyonge kwenye mbio za ubingwa dhidi ya Yanga? Na je? Yanga atakubali ubingwa uchukuliwe mbele ya macho yake ni jambo la kusubiri wakati Miamba hao watakapo kutana kufanya maamuzi wenyewe.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment