Muhsini Malima Ametua Rasmi Azam FC, Aahidi Makubwa kwa Mashabiki

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Dar es Salaam – Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji mahiri Muhsini Malima kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Zed FC ya nchini Misri, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Malima, ambaye hajapata nafasi ya kucheza mechi yoyote akiwa na Zed FC, amejiunga rasmi na Azam FC baada ya kushiriki zoezi la picha rasmi za utambulisho ("photoshoot") na klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi, Dar es Salaam.

Kabla ya kujiunga na Zed FC, Malima alikuwa mchezaji wa Dodoma Jiji FC, klabu iliyomlea na kumpa nafasi ya kung’aa hadi kuvutia macho ya timu za nje ya nchi. Hata hivyo, kurejea kwake nyumbani Tanzania kumetajwa kama fursa mpya ya kufufua makali yake katika soka la ushindani.



Azam FC imeweka matumaini makubwa kwa mshambuliaji huyo chipukizi, ambaye anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayopania kurudisha heshima yake katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.


0767915473

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments