Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kama Kariakoo Derby, kati ya Young Africans na Simba SC unatarajiwa kupigwa Jumatano, tarehe 25 Juni 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, maandalizi ya mchezo huo mkubwa tayari yamekamilika huku maofisa wa mchezo namba 184 wakithibitishwa rasmi.
Mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa Amin Mohamed Amin Omar kutoka Misri, akisaidiwa na waamuzi wasaidizi wawili: Mahmoud Ahmed Abo El Regal na Samir Gamal Saad Mohamed, wote kutoka Misri, Mwamuzi wa nne atakuwa Ahmed Mahrous Elgandour pia kutoka Misri, huku Salim Omary Singano kutoka Tanga akiwa Kamishna wa mchezo huo.
Msimamizi wa waamuzi (Referees Assessor) ni Alli Mohamed kutoka Somalia, jambo linalodhihirisha ukubwa wa mechi hiyo hadi kuhitaji maofisa wa kimataifa kusimamia haki na usawa.
Mchezo huo unatarajiwa kuvuta maelfu ya mashabiki kutoka kona mbalimbali za nchi, huku kila timu ikisaka heshima na alama muhimu kuelekea kumalizika kwa msimu wa ligi, Kariakoo Derby daima imekuwa kivutio kikubwa nchini kutokana na ushindani mkali wa kihistoria kati ya timu hizi kongwe na zenye mashabiki wengi zaidi Tanzania.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment