Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa haina mpango wa kumsajili kipa wa timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martínez, katika dirisha hili la usajili.
Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, miamba hiyo ya soka nchini Uingereza imesema haitahusiana na dili lolote la kumleta golikipa huyo wa Aston Villa, licha ya tetesi kusambaa kwamba klabu hiyo ilikuwa inamnyatia.
Martínez, ambaye amekuwa mmoja wa makipa bora barani Ulaya kutokana na uchezaji wake wa kuvutia na mchango mkubwa katika mafanikio ya Argentina ikiwemo ubingwa wa Kombe la Dunia 2022, sasa haipo tena katika mipango ya Manchester United.
Klabu hiyo inayojulikana kama Mashetani Wekundu, imeelekeza nguvu zake katika maeneo mengine ya kikosi chake huku ikitarajia kuendelea na huduma za kipa wao namba moja, André Onana kwa msimu ujao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment