Timothy Lugembe,
mwanakwetusports .
Licha ya kutangazwa kushushwa daraja kwa sababu ya hali mbaya ya kifedha, klabu ya Olympique Lyonnais imejumuishwa kwenye ratiba rasmi ya msimu ujao wa Ligue 1 nchini Ufaransa.
Ratiba hiyo iliyotolewa Ijumaa inaonyesha kuwa Lyon wamepangwa kucheza dhidi ya Lens katika mchezo wao wa ufunguzi wa msimu wa 2025/2026 utakaopigwa kati ya tarehe 16 na 17 Agosti. Hii inajiri licha ya klabu hiyo kubwa kushushwa daraja kwa muda tangu Novemba mwaka jana na chombo cha usimamizi wa fedha cha vilabu vya soka nchini Ufaransa DNGC.
Uamuzi huo ulitokana na hali tete ya kifedha ya klabu hiyo, ambapo wamiliki wake, Eagle Football Group wakiongozwa na mfanyabiashara John Textor, walitangaza kuwa Lyon inakabiliwa na deni la pauni milioni 422 kufikia Oktoba mwaka jana. Hali hiyo ilipelekea DNGC kutangaza kuwa klabu hiyo haina uwezo wa kifedha kuendelea kushiriki ligi kuu.
Hata hivyo, maafisa wa Lyon, akiwemo Textor, walikutana tena na DNGC wiki hii kujaribu kuonyesha hatua walizochukua kuboresha hali ya kifedha lakini walishindwa kuishawishi taasisi hiyo kubatilisha adhabu ya kushushwa daraja. Pamoja na hayo, klabu hiyo maarufu kwa jina la “Les Gones” imekata rufaa kupinga uamuzi huo huku ikiutaja kama “haueleweki.”
Iwapo Lyon wataendelea kujumuishwa kwenye Ligue 1 huku bado wakikabiliwa na zuio la kifedha, huenda likazua mvutano mkubwa ndani ya UEFA na vyombo vya soka barani Ulaya kuhusu kanuni za umiliki wa klabu nyingi.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment