LIONEL MESSI AFUFUA MATUMAINI YA INTER MIAMI KATIKA KOMBE LA DUNIA LA KLABU

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Nahodha wa Inter Miami, Lionel Messi, ameibuka shujaa kwa kuiongoza timu yake kupata ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya FC Porto kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA Club World Cup).

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, FC Porto walipata bao la kuongoza dakika ya 8 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Samu Aghehowa baada ya VAR kuthibitisha madhambi ya beki wa Inter Miami,  dakika ya 47 Miami walisawazisha kupitia Segovia na dakika ya 54 Lionel Messi alifunga bao la pili kupitia mpira wa kutenga na kutengeneza mtumaini kwa Miami kufuzu hatua ya makundi.

Kwa ushindi huo, Inter Miami wamefikisha alama 4 sawa na Palmeiras katika Kundi A, na kuweka nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali, Mchezo wao wa mwisho wa kundi utakuwa dhidi ya Palmeiras, huku ushindi au sare ukiwapa nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.

 

 

0/Post a Comment/Comments