Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Msimu wa 2024/2025 wa Ligi Kuu Tanzania Bara umefikia tamati huku matukio makubwa yakishuhudiwa kwenye viwanja mbalimbali nchini, ikiwemo kushuka kwa timu mbili daraja na pambano la ubingwa kati ya watani wa jadi Simba na Yanga linalotarajiwa kuchezwa Jumatano June 25 mwaka huu.
Katika matokeo ya mwisho ya msimu, Kagera Sugar na KenGold FC wameshuka daraja rasmi baada ya kumaliza ligi wakiwa nafasi ya 15 na 16 mwiahoni mwa msimamo wa ligi na rasmi msimu ujao watacheza championship .
Kwa upande mwingine, timu za Tanzania Prisons na Fountain Gate FC zitatakiwa kupambana katika hatua ya mtoano (playoff) dhidi ya timu mbili kutoka Championship ili kujua hatima yao ya kubaki au kushuka daraja.
Katika kilele cha msimu, pambano kubwa linatarajiwa Jumatano, wakati Simba SC na Yanga SC watakapomenyana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa mwisho wa ligi. Yanga wanaongoza ligi kwa pointi 79, wakati Simba wakifuatia kwa pointi 78, hali inayofanya mechi hiyo kuwa ya kuamua bingwa wa msimu huu. Sare yoyote kwa Yanga itawatosha kutwaa ubingwa kwa mara nyingine mfululizo.
Katika michezo Yao ya mwisho Simba ilishinda 1-0 dhidi ya Kagera sugar huku Yanga wakishindwa 5-0 dhidi ya Dodoma jiji , Mashabiki wa soka nchini na nje ya mipaka wanaelekeza macho yao kwenye derbi hii ya kukata na shoka, inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa na yenye mvuto wa kipekee.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment