JKT QUEENS WATWAA UBINGWA WA TWPL MGUTO ATOA NENO.

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports,

TIMU ya mpira wa miguu wanawake JKT Queens wamebeba ubingwa wa ligi hiyo kwa mwaka wa mashindano 2024/2025 baada ya kuongoza ligi hiyo wakiwa na point 41sawa sawa na Simba Queens kilicho tofautisha ni magoli ya kufunga na kufungwa kitu kilicho wapa ubingwa JKT.

Makamu wa pili wa raisi Steven Mguto ameisifu Timu hiyo kwa kuchukua ubingwa wakiwa na Timu ya kizalendo yaani wachezaji wazawa ambao wameweza kuchuana na wachezaji wakigeni kutoka Simba na yanga na kufanikiwa kuchukua kikombe hicho.

Pia ameuomba uongozi wa JKT kuendeleza kuwalea vijana hao ili kukuza vipaji vyao na anaamini kuwa kwenye mashindano ya kimataifa ambayo watakwenda kuwakiliasha anatarajia wafike hatua angalau ya fainali tofauti na msimu ulio pita ambao walitolewa mapema.

Kwa upande wa kocha wa JKT Queens Ester Chabruma amesema kuwa wamechukua ubingwa lakini msimu huu ulikuwa ni mgumu sana huku changamoto kubwa wakiipata kutoka kwa Simba ,yanga na baadhi ya michezo ya mikoani na ameahidi kuwa msimu ujao waendelea walipo ishia ili kutetemeka ubingwa wao

Kwa upande wa ubora wa ligi hiyo Ester amesema kuwa ligi inakuwa ukilinganisha msimu uliopita na msimu huu kunamabadiliko makubwa hususani kiushindani timu zinazidi kuimarika na kuleta changamoto Cha muhimu timu kufanya maandalizi ya kutosha.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments