Timothy Lugembe ,
Mwanakwetusports.
Jacob Masawe, nahodha wa Namungo FC, amekuwa akionyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania, kwa misimu mingi mchezaji huyo anae cheza nafasi ya kiungo wa kati amekuwa nahodha wa timu zzote alizo pitia ikiwemo Toto Africa, Gwambina FC, na sasa Namungo.
Masawe ameelezea kiu yake ya kuitumikia timu ya Taifa baada ya kikosi kuitwa na yeye hakujumuishwa amesema kuwa anahitaji kutoa mchango wake katika timu hiyo na ameongeza kuwa kuwa Kila mmoja anatamani kuitumikia timu ya Taifa na kwa upande wake yupo tayali wakati wowowte atakapo hitajika .
Licha ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye nafasi ya dimba lakati lakini hajawahi kujumuishwa kwenye timu ya Taifa (Taifa stars) kwa misimu yote tangu ameanza Kusakata kabumbu, imekuwa ni ngumu kwa Jacob Masawe kujumuishwa kwenye timu ya Taifa kwasababu timu hiyo imejaa viungo wengi sana na wenye uzoefu mkubwa ndio maana imekuwa ngumu kwake yeye kujumuishwa kutokana na ushindani huo.
Mara nyingi kwenye soka kote ulimwenguni mchezaji anaweza kuwa na kiwango bora sana lakini asipate nafasi ya kuichezea timu ya Taifa hiyo ni kutokana na nafasi anayocheza wakati huo inaushindani kiasi gani na muda mwingine inaangaliwa ni timu gani unacheza.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment