HESHIMA KWA TAIFA MWALIMU MTANZANIA WA KWANZA KUCHEZA CLUB WORLD CUP

  


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika hatua ya kihistoria kwa soka la Tanzania, Selemani Mwalimu ameweka rekodi mpya kwa kuwa MTanzania wa kwanza kushiriki mchezo wa FIFA Club World Cup, Mwalimu alicheza katika mechi dhidi ya Juventus ambapo timu yake ilikubali kichapo cha mabao 4-1, lakini tukio hilo limeandika historia kwa taifa lake.

Mwalimu aliingia uwanjani katika dakika ya 46, akichukua nafasi ya Bart Meijers, Ingawa matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wao, lakini ushiriki wake katika michuano hiyo mikubwa duniani ni mafanikio makubwa kwa mchezaji binafsi kwani.inamuongezea wasifu binafsi katika maisha yake ya uchezaji na pia ni heshima kwa Taifa .



FIFA Club World Cup ni moja ya mashindano ya hadhi ya juu duniani kwa ngazi ya vilabu, ambapo mabingwa wa mashindano ya mabara hukutana kuwania taji la dunia, Ushiriki wa Mwalimu ni dalili ya ukuaji wa vipaji kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla na hii ndio maana halisi ya kukua kwa soka la Tanzania.

Wananchi na wadau wa soka nchini wamempongeza Mwalimu kwa hatua hiyo muhimu, wakimtaja kama mfano wa kuigwa kwa wachezaji chipukizi nchini wanaotamani kufika mbali katika soka kuiga juhudi na upambanajinwa mwalimu.

0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments