Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha maarufu wa kandanda, Gennaro Gattuso, anatarajiwa kusaini mkataba rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia, Azzurri, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati yake na Shirikisho la Soka la Italia (FIGC).
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Gattuso tayari amekubali masharti ya mkataba huo na anatarajiwa kutambulishwa rasmi wiki hii, Hatua hii inakuja kufuatia juhudi za FIGC kuboresha kiwango cha timu hiyo kuelekea mashindano yajayo ya kimataifa ikiwemo kombe la dunia 2026.
Gattuso, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azzurri na mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2006, ana historia ya mafanikio akiwa mchezaji na pia kocha katika vilabu mbalimbali vya Italia na Ulaya. Uteuzi wake unatazamwa kama mwanzo mpya kwa kikosi cha Italia, ambacho kimekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika benchi la ufundi.
Mashabiki wengi wa soka nchini Italia na duniani kote wanatarajia kuona namna Gattuso atakavyorejesha hadhi ya Azzurri na kuwapa ushindani katika michuano mikubwa kama Euro na Kombe la Dunia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment