Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Uhamisho wa Florian Wirtz kwenda Liverpool, sasa umekamilika rasmi, na umekuwa gumzo kubwa katika ulimwengu wa soka kwa wiki kadhaa zilizopita.
Kiungo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye alitwaa ubingwa wa Bundesliga bila kupoteza mchezo na Bayer Leverkusen msimu wa 2023-24, chini ya kocha Alonso sasa amejiunga rasmi na Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wake uliosubiriwa kwa hamu, na mashabiki wa timu hiyo.
Kufika kwake Anfield ni hatua mpya katika safari yake ya soka ambayo imemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye mvuto mkubwa na wanaowindwa zaidi barani Ulaya akiwa na umri wa miaka 22 tu na anatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchezaji klabuni hapo.
Steven Gerrard aliyekuwa nahodha wa timu ya Liverpool alipata wasaha wa kumzungumzia Wirtz ambapo amesema kuwa mchezaji huyo akiwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja uwerevu na nidham havipishani.
"Kila siku, alivyo nje ya uwanja ndivyo alivyo ndani ya uwanja, Anavutia sana, Anacheza kana kwamba amekuwa akicheza kwa miaka 10. Ni mwerevu Pia ni mtu mzuri sana Alikuwa wa kwanza kunijali nilipowasili kwenye klabu [Leverkusen], alikuwa rafiki yangu wa kwanza. Writz aliniuliza kuhusu Celtic, alinikaribisha nyumbani kwake, tulikuwa tunatoka pamoja kwa chakula cha jioni. Alifanya mambo ambayo yalinifanya nijisikie niko nyumbani"
Kila lakheri kwa mshambuliaji Writz katika maisha yake ya soka akiwa na klabu ya Liverpool.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment