FIFA YAFAFANUA UTARATIBU HATARI YA RADI MCHEZONI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa mwongozo rasmi unaolenga kulinda usalama wa wachezaji, maofisa wa mechi na mashabiki dhidi ya hatari za radi wakati wa michezo.

Taarifa hii imekuja mara baada ya kuwepo na mfululizo wa mchafuko wa Hali ya hewa kwenye baadhi michezo na wakati wa mazoezi ambapo radi zimekuwa zipiga na kuhatarisha usalama , Moja ya matukio hayo ni mchezo wa Benfica vs Chelsea ambapo wachezaji na Mashabiki walitolewa uwanjani kwaajili ya usalama wao ambapo Chelsea walishinda 4-1.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, FIFA inasisitiza kwamba mchezo wowote wa soka lazima usimamishwe au ucheleweshwe kwa angalau dakika 30 endapo radi itapigwa karibu na uwanja, hasa ikiwa itatokea ndani ya mduara wa maili 10 (sawa na takribani kilomita 16) kutoka eneo la mchezo.

Taarifa hiyo ya kiusalama imeeleza kuwa mara tu radi inapogunduliwa ndani ya umbali huo hatarishi, waamuzi au waangalizi wa mechi wanapaswa kuagiza kuondoka kwa haraka kwa wachezaji na maofisa uwanjani na mchezo hauwezi kurejelewa hadi baada ya muda huo kupita bila radi nyingine kupiga tena.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za FIFA kuhakikisha afya na usalama vinatangulizwa wakati wa mashindano, hasa katika mazingira yenye hali ya hewa isiyotabirika.

Mashabiki na wadau wa soka duniani kote wanahimizwa kuelewa na kuheshimu miongozo hii, hususan katika mashindano makubwa kama FIFA Club World Cup na Kombe la Dunia ambapo mechi kadhaa hivi karibuni zimewahi kucheleweshwa kwa sababu ya radi

0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments