Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashindano ya FIFA Club World Cup 2025 yanayoendelea nchini Marekani yamegeuka jukwaa la ubabe wa soka kwa vilabu vya Brazil, huku timu za Afrika zikipoteza mwelekeo na kubaki kuwa watazamaji wa mafanikio ya wenzao , huku Timu kutoka Brazili zikiwashangaza wengi kwa kufanya vizuri.
Kwa mara ya kwanza mashindano haya yamehusisha vilabu 32 kutoka mabara yote, yakifanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai 13. Timu za Brazil zikiwemo Flamengo, Fluminense, Botafogo na Palmeiras zimeonyesha kiwango cha juu kilichowaacha wengi mdomo wazi, Mchezo wa kasi, nidhamu ya hali ya juu, na ubunifu wa hali ya juu umeifanya samba ya Brazil kutikisa mashindano haya.
Fluminense imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, huku Palmeiras ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri. Botafogo na Flamengo nao hawakubaki nyuma, wakipata ushindi mkubwa dhidi ya PSG na Chelsea vilabu vikongwe kutoka Ulaya.
Kwa upande wa Afrika, mambo hayajawa mazuri Wawakilishi kama Al Ahly, Experence Wydad, na Mamelodi Sundowns wamepambana kwa hali na mali, lakini wamejikuta wakikosa makali mbele ya vigogo wa soka duniani kwa kuondoshwa hatua za makundi , Makocha na mashabiki wameeleza kuwa hali hiyo inatokana na ukosefu wa maandalizi ya kutosha, miundombinu hafifu, na uzoefu mdogo wa kimataifa na ubora wa wachezaji.
Wakati huu fainali ikisubiriwa kuchezwa Julai 13 , ulimwengu unajiuliza, je, Brazil wataendeleza moto wao hadi kutwaa taji, au Ulaya itarejesha hadhi yake? Afrika kwa sasa, imesalia kutazama kwa matumaini .
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment