Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports,.
Muda mchache ujao Timu ya FC Barcelona ya nchini Hispania itaanza mazungumzo na beki wa timu ya Arsenal ya nchini Uingereza Thomas Partey ambaye mkataba wake unatarajia kuisha mwishoni mwa mwezi huu.
Timu ya Arsenal tayali imetoa ruhusa kwa mchezaji huyo kuanza mazungumzo na Timu yoyote na ataondoka kwenye kikosi hicho kama mchezaji huru, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuanza mazungumzo na Barcelona ili kuangalia uwezekano wa mchezaji huyo kuweza kujiunga na timu hiyo.
Lakini FC Barcelona wamevutiwa zaidi na mchezaji huyo kwasababu ya uzoefu alionao ukilinganisha na wachezaji walipo kikosini hapo hawana uzoefu wakutosha hivyo ataongeza uzoefu kingine ni mchezaji imara ambaye anaondoka kama mchezaji huru hivyo timu hiyo ikimsajili watakuwa wamepunguza gharama na kukwepa changamoto ya financial Fair play ambayo imekuwa ikiwatesa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment