Chelsea Yasajili Kipaji Chipukizi Mamadou Sarr kutoka Ufaransa

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Chelsea imetangaza kumsajili beki chipukizi Mamadou Sarr, akitokea Strasbourg ya nchini Ufaransa mchezaji huyo amejiunga rasmi na The Blues na anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo kwa miaka ijayo.

Mamadou Sarr, ambaye pia ni sehemu ya timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa, amekuwa akivutia macho ya vilabu vikubwa barani Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzuia, kasi, na uelewa wa mchezo licha ya umri wake mdogo. Akiwa na maumbile ya kimichezo na nidhamu ya hali ya juu, Sarr anachukuliwa kama mmoja wa mabeki wenye mustakabali mzuri katika soka la kisasa.

Kupitia ujumbe rasmi wa klabu, Chelsea ilimkaribisha mchezaji huyo kwa maneno,"Welcome to Chelsea, Mamadou Sarr" ikielezea furaha yao kwa kumpata beki huyo mwenye kipaji.

Usajili huu unaonyesha dhamira ya Chelsea kuendelea kuwekeza kwa wachezaji vijana kwa lengo la kujenga kikosi imara kwa ajili ya mafanikio ya baadaye, mashabiki wa Chelsea kote duniani wanasubiri kwa hamu kumuona Sarr akionyesha uwezo wake katika dimba la Stamford Bridge.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments