Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la mpira wa miguu Africa CAF limetoa utaratibu kuhusu michuano ya Timu za Taifa kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN yanayoandaliwa na nchi tatu Tanzania, Kenya, na Uganda mashindano yanatarajiwa kuanza Agosti 2025.
Kupitia barua ya CAF kwa TFF imeelezea ratiba nzima kuanzia vituo ambavyo michezo itafanyika , katika barua hiyo Tanzania imepewa nafasi ya kuandaa mchezo wa ufunguzi wakati nchi ya Uganda ikipewa nafasi ya kuandaa mchezo wa mshindi wa tatu na fainali kufanyika nchini Kenya
Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa ufunguzi wa michuano mikubwa walishawahi kupewa nafasi ya kuandaa ufunguzi wa AFRICAN FOOTBALL LEAGUE Katika uwanja wa Benjamin mkapa na ufunguzi ulifaana huku ukihudhuriwa na watu waheshima kwenye soka akiwemo raisi wa mpira wa miguu Duniani Gianni Infantino , rais wa CAF Patrice Motsepe na Arsene Wenge.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment