Timothy Lugembe.
Mwanakwetusports.
Mashindano ya African Nations Championship (CHAN) 2024 yatakayoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya, Tanzania, na Uganda yamewekwa katika ramani rasmi huku droo ya hatua ya makundi ikionesha Tanzania iko kwenye Kundi B lenye ushindani mkubwa.
Taifa Stars itaanza kampeni yake kwa kuvaana na Burkina Faso katika mchezo wa Ufunguzi utakao fanyika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, Agosti 2, 2025.
Mashindano haya ambayo yanashirikisha wachezaji wa ligi za ndani pekee ni jukwaa halisi la kuonesha ubora wa ligi mbalimbali barani Afrika, Kwa Tanzania, CHAN 2024 ni kipimo kikubwa kupima ubora wa Ligi Kuu ya NBC, ikizingatiwa kuwa timu nyingine katika kundi hilo ni Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kwa upande mwingine, kundi A lina vigogo kama Kenya, Morocco, Angola, DR Congo na Zambia, huku kundi C likiwa na Niger, Uganda, Guinea, Algeria na South Sudan, ambalo michezo yake itapigwa jijini Kampala, Uganda. , na kundi D likiwa na Timu za Senegal, Congo, Sudan na Nigeria.
Uwanja wa Benjamin Mkapa utatumika kama uwanja wa nyumbani kwa Taifa Stars, huku Amaan Stadium Zanzibar, ukiwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kwa baadhi ya michezo ya kundi C.
Kwa wapenzi wa soka wa Tanzania, CHAN 2024 ni zaidi ya mashindano ni jukwaa la kupima juhudi za maendeleo ya soka la ndani, kuonesha vipaji na kuwapa nafasi wachezaji wa nyumbani kupata uzoefu wa kimataifa.
Je, Ligi Kuu ya Tanzania iko tayari kushindana kwa ubora na ligi zingine Afrika? CHAN 2024 italeta majibu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment