Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa kwanza wa kufungua mashindano ya club world cup nchini Marekani uliowakutanisha timu ya Al Ahaly ya misri dhidi ya Inter Miami ya Marekani katika uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens umemalizika kwa Timu hizo kutoshana nguvu ya bila kuungana.
Katika mchezo huo wa Kundi A, Al Ahly walionyesha ubora kipindi cha kwanza na walikosa bao baada ya penalti ya Trezeguet kuokolewa na kipa Óscar Ustari wa Miami, Kipindi cha pili kilishuhudia Inter Miami ikiongeza kasi huku nyota wao Lionel Messi akikosa mabao mawili ya wazi, ikiwemo mpira wa adhabu uliogonga mwamba.
Mashabiki zaidi ya 60,000 walifurika kushuhudia mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua licha ya kutofungika kwa bao.
Inter Miami watakutana na FC Porto kwenye mechi yao ijayo, huku Al Ahly wakijiandaa kumenyana na Palmeiras mechi zote zitachezwa Juni 19.mwaka huu.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment