Na Timothy Lugembe
Mwanakwetu Sports
Selemani Mwalimu Abdallah ni mchezaji wa soka wa Tanzania anayecheza nafasi ya mshambuliaji wa kati. Alizaliwa tarehe 19 Januari 2006 na kwa sasa ana umri wa miaka 19. na anachezea klabu ya Wydad Athletic Club (WAC) ya Morocco, mojawapo ya klabu kubwa barani Afrika.
Kabla ya kujiunga na wydad Casablanca ya nchini moroko mwalim alikuwa mchezaji wa Fountain gate ambako alikuwa akicheza kwa mkopo kutokea Timu ya Singida black stars zote zikishiliki liguu ya Tanzania bara (NBC premier league) baada ya kuonyesha kiwango Bora kwa msimu wa 2024/2025 kwa kufunga magoli 6 katika michezo 11 ndipo Wydad wakamuona na kumsajili kwa mkataba wa miaka mi nne na nusu wenye thamani ya takribani million 891 za kiTanzania.
Mwalim anatarajiwa kuwa Mchezaji MTanzania wa kwanza kushiriki mashindano ya vilabu duniani ( Club word cup) baada ya Timu yake kupata tiketi ya kushiri mashindano hayo kama akifanikiwa KUCHEZA mchezo hata mmoja atakuwa ndio mchezaji wa kwanza wa kiTanzania kushiriki MICHUANO hiyo toka kuanzishwa kwake.
Mashindano ya club word cup yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia TAREHE 15 mwenzio wa sita mpaka Tarehe 13 mwez wa Saba mwaka huu nchini Marekani na viwanja 11 vipo tayali kwaajili michezo hiyo viwanja vitakavyo tumika ni pamoja na Rose Bowl stadium, MetLife stadium, Mercedez-Benz arena, Lincoln Financial field, Lumen field, Hard rock stadium, Camping world stadium, Geodis park, TQL stadium, Aud field, pamoja na bank of America stadium.
Post a Comment