Na Timothy Lugembe,
Mwanakwetu Sports.
Timu ya Real Madrid ya nchini Hispania imeshindwa kufanikiwa mpango wake wa kumsajili mchezaji wa Liverpool ya nchini Uingereza Trent Alexander Arnold kama mchezaji huru hii imetokana na kuwepo kwa mashindano ya club world cup yanayo tarajiwa kuanza Tarehe 15 mwezi wa sita mwaka huu.
Mkataba wa mchezaji huyo ulikuwa unatarajia kuisha mwezi wa sita mwaka huu lakini kutokana na kuanza kwa mashindano hayo imekuwa ni ngumu kwa Timu hiyo kusubiri mpaka mkataba uishe kutokana na kuhitaji huduma ya mchezaji huyo yote hiyo ni kutokana majeruhi yaliyo wakumba wachezaji wao wa kikosi Cha kwanza.
Timu ya Real Madrid imemsajili Trent Alexander Arnold kwa kiasi Cha £ 10M (Euro million kumi) kutokana na mkataba wa mchezaji huyo kubakiza mwezi mmoja ambao ungetamatika Tarehe 30 mwezi wa sita mwaka huu.
Imekuwa ni tabia ya Timu ya Real Madrid kusajili wachezaji waliomaliza mkataba Yao ili kupunguza gharama za kusajili mfano wawachezaji ghari waliosajiliwa na Timu hiyo bure ni pamoja na Kylian Mbappe kutoka PSG, na kwa sasa wamekwama kumsajili Trente kutokana na kuwahi kwa mashindano ya club world cup.
lugembetimothy@gmail.com
Post a Comment