JEAN CHARLES AHOUA KIPAJI HALISI KUTOKA GHANA

 


Na Rashid Msiri

Mchezo wa soka ni zaidi ya udugu ni Zaidi ya simulizi za mapenzi na hadithi za tamu kwa wapendanao ni Zaidi hata furaha ya binti aliyeahidiwa kununuliwa toleo jipya la gari analolipenda na mwenza wake,

Je uliwahi kuwaza furaha ya shabiki wa mchezo wa soka pale timu anayoishabikia kwa inapofanya vizuri katika michuano mikikubwa inayoshiriki ? hii inasadifu zaidi ya maisha na utamu wa masimulizi wa hekaya za abunusi ama hadithi za kibanga kumpiga mkoloni.

Ni Zaidi ya Maisha, Ni Zaidi ya mapenzi Kwa nyota wa Klabu yao pendwa, Ni Zaidi ya furaha ya mwanasiasa kuhutubui na kupambania wananchi anaowatetea, hivi uliwahi kuwaza mapenzi ya mashabiki wa FC Barcelona kwa nyota wao Lamine Iyamal au hisia walizonazo mashabiki wa national al ahaly kwa gwiji wa klabu Mohammed Aboutrika ?

Leo Nimetaka visa hadi pwani ya Ivory coast pwani ambayo imejaa mengi masimulizi kwa vizazi na vizazi juu ya masimulizi ya vipaji na umashuhuri wa magwiji wa kubwa wa mchezo wa soka waliowahi kuitumikia Timu ya taifa Hiyo ya Tembo wa Afrika.

Mnamo mwaka 2002 katika mji wa Lôh-Djiboua alizaliwa kijina mwenye kipaji kibwa cha kusakata kabumbu, nyota yake ilianza kung’aa mapema akiwa kinda kwenye Timu ya soka ya LYS Sassandra kama nyota kutokea kwenye soka la vijana kwani klabu hiyoilikuwa bado ni mpya kwa watu wengi nchini Ivory coast na Afrika kwa ujumla ila kipaji chake kiliwavutia maboss wa klabu hiyo na kumpa nafasi katika kikosi cha klabu hiyo.

Kutokana na ubora na upekee wa kipaji chake ambacho kiliwashangaza wengi ndipo klabu Séwé Sports ilivutiwa naye na mnamo Julai 2020 viongozi wa klabu hiyo waliamua kumsajili nyota huyo ambapo hapa alicheza kwa kiwango kizuri kilichovutia miamba ya soka kwa upande ndani nchi Ivory coast na Mnamo Julai 2022, alihamia Stella Club d’Adjamé, ambapo alionyesha kiwango cha juu na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) wa Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu wa 2023/2024, baada ya kufunga mabao 12 na kutoa pasi 9 za mabao.


Uwezo wake wakulisakata kabumbu ulivutia vilabu vingi Afrika ndipo magwiji wa soka nchini Tanzania Simba Sports Club uliinasa Saini ya nyota huyo ambaye amejaa utulivu na ustadi mkubwa katika kulisakata kabumbu, na ufundi alionao katika eneo la ubunifu wakutengeneza nafasi ndio chanzo kikubwa kilichowavutia watu wengi .

Jean Charles Ahoua huyu ni mwanandinga ambaye Jean Charles Ahoua , katika msimu uliopita akiwa na Klabu ya stellaclubdadjame , alifunga mabao 12 na kutoa asisti 9, na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi ya Ivory Coast katika kipindi cha miaka minane iliyopita.

Julai 2024, Ahoua alisajiliwa na Simba SC, Katika msimu wake wa kwanza, tayari amefunga mabao 15 na kutoa asisti 7.


Ahoua amehusika moja kwa moja katika mabao 22 kwenye Ligi Kuu ya NBC—zaidi ya mchezaji mwingine yeyote.

Huyu ni nyota ambaye ameamua kuacha namba zazke za ubora kwa takwimu ziamue Zaidi juu ya kiwango, nimchezaji ambaye si mwingi wa mbwembwe uwanjani, si mwingi wa chenga ila ameamu miguu yake izungumze mpira katika upande wa magoli ila Jean Charles Ahoua MVP wa ligi ya Ivory coast msimu uliopita na Nyota wa kutegemewa kwenye kikosi cha Simba Hatimaye ameaanza kusaka Tuzo nyingine ya MVP akiwa Tanzania.

Baada ya kuondoka clatous Chama ndani ya Simba Sports Club klabu hiyo ilimsaili Jean Ahoua kama mbadala wake lakini watu wengi walikuwa hawajaelewa juu ya uchezaji wake ila Ubora wake umeanza kuwavutiavwatu wengi ndani ya klabu ya soka ya Simba.


Goli la Jean Charles Ahoua zidi ya Stellenbosch ya Afrika kusini katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika katika hatua ya nusu fainali hii itabikia ni historia katika mioyo ya wanasimba kwani ni goli lililowapeleka Simba katika hatua ya fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa upande wa vilabu baada ya miaka 30 kupita tangu kufika hatua kama hiyo ya michuano ya vilabu barani Afrika.

Simba sports club ni moja kati ya ambazo kwa miaka mingi imekuwa ikijipambanua kama klabu inayotoa nafasi kwa wachezaji mbalimbali kuitumia kama daraja wanapofanya vizuri wapo tayari kuwaachia waweze kwenda kutafuta marisho yaliyo bora Zaidi nje ya klabu hiyo sahau kuhusiana na Pape Osman Sakho, sahau kuhusu Clatous Chama, sahau kuhusiana Emmanuel Okwi, sahau kuhusiana na Luis miquissone na sahau kuhusiana Mbwana Ally Samatta,


 Jean Charles Ahoua anaweza kuwa mmoja wa wanandinga ambao wanaweza kuitumia klabu hiyo kama daraja kwenda sehemu nyingine yenye malisho bora Zaidi barani Afrika ama barani ulaya kama vile alivyowahi kuitumia fursa hiyo Pape Osman Sakho ?


0/Post a Comment/Comments