HISTORIA YA FAINALI UEFA KATI YA PSG NA INTER MILLAN

 


Na Timothy Lugembe,

Mwanakwetu Sports,

Paris Saint-Germain (PSG) hii ni mara ya pili kwa PSG kufika fainali ya UEFA Champions League. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2020, ambapo walifungwa bao Moja bila na Timu ya Bayern Munich, Hadi sasa Timu ya PSG hawajafanikiwa kuchukuwa ubingwa huo na wanatatajiwa kutupa karatayao hii Leo kwenye fainali Yao ya pili toka kuanzishwa kwake.

Timu ya Inter Milan Hii ni fainali yao ya saba katika mashindano haya na Wametwaa taji hili mara tatu (1964, 1965, na 2010). Mara ya mwisho kufika fainali ilikuwa mwaka 2023, ambapo walifungwa na Manchester City kutokea nchini Uingereza kwa bao Moja kwa bila.

PSG na Inter Milan hawajawahi kukutana katika mechi ya ushindani rasmi kabla ya fainali hii. Mikutano yao ya awali ilikuwa katika mechi za kirafiki, ikiwa ni pamoja na Desemba 31, 2014, PSG 1–0 Inter Milan , Desemba 30, 2015 Inter Milan 0–1 PSG, Julai 24, 2016 Inter Milan 1–3 PSG (International Champions Cup), Julai 27, 2019 PSG 1–1 Inter Milan (Inter walishinda kwa mikwaju ya penalti 6–5) , Agosti 1, 2023: PSG 1–2 Inter Milan. Katika michezo hiyo PSG amefanikiwa kushinda michezo mitatu sare Moja huku Inter wakishindwa mchezo mmoja je PSG wataendeleza u babe kwa inter?

Mchezo wa Leo hii unatarajia kufanyika nchini ujerumani katika dimba la Allianz arena majira ya saanne kamili usiku kwa saa za Africa mashabiki.



0767915473

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments