FERNANDO BAPTISTA DE SEIXAS PEYROTEO DE VASCONCELOS

Na Rashid Athumani

Sahau kuhusiana na
Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, anayejulikana zaidi kama Cristiano Ronaldo au CR7, ambaye ni mchezaji wa soka wa Ureno anayetambulika kimataifa kwa mafanikio yake makubwa katika uwanja wa soka. Akiwa nimzaliwa wa tarehe 5 Februari 1985 katika mji wa Funchal, kisiwa cha Madeira, Ureno.

Ronaldo alikulia katika familia ya kipato cha chini akiwa mtoto wa nne na wa mwisho wa Maria Dolores dos Santos na José Dinis Aveiro. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa klabu ya soka ya CF Andorinha, ambapo Ronaldo alianza kucheza soka akiwa na umri mdogo. Baadaye alijiunga na klabu ya Nacional kabla ya kuhamia Sporting CP, ambapo alionyesha vipaji vyake vya kipekee na kuvutia vilabu vikubwa barani Ulaya na dunia kwa ujumla .

Katika taifa la Ureno kuna nyota wengi wakubwa waliowahi kufanya mengi yanayosimulia vizazi na zizazi ila lipo jina moja ambalo limekuwa na mengi yakusimuliwa kwa viazi huku wengi wakienda mbali na kusema yeye ni Bora wa muda wote katika taifa la ureno.

Sahau kuhusiana na fundi wenye asili ya kiafrika nchi ya msumbiji ambaye amefanya makubwa barani ulaya akiwa na klabu ya Benfica miaka ya 1942 Eusébio da Silva Ferreira ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 1966 akiwa na mabao 9 vile mwaka mmoja nyuma aliwahi kutwa tuzo ya Ballon Dor 1965, pia sahau kuhusiana na historia bora ya nyota kama Luis Figo, Rui Costa, Ricardo Carvalho, Ila Ipo nyota ambayo imetajwa kwenye masimulizi ya vitabu na majarida yaliyojaa kumbukumbu kubwa juu ya mchezo wa soka Ikilitaja Jina moja kuwa Na thamani mfano wa alamasi kutokea mkoani shinyanga ama Tanzanite kutokea palepale Mererani.

Mnamo mwaka 1918 katika nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na hifadhi kubwa ya almasi barani Afrika Angola katika mji wa Humpata ikiwa bado nchi hiyo ipo katika zama za ukoloni wakitawaliwa na taifa la ureno alizaliwa kijana aliyejawa na historia isiyo na mfano katika masimulizi,

Pepo za bahari kutoka bahari ya hindi zinanisafirisha Zaidi ya Kilomita 2879 ndani ya taifa la Angola mnamo tarehe 10 march 1918 alizaliwa gwiji Fernando Baptista de Seixas Peyroteo de Vasconcelos ama kwa ufupi unaweza kumuita Fernando Peyroteo ambaye alikuwa na asili ya kizungu kutokana na kuzaliwa na wazazi wote wawili wenye asili ya kireno kutoka kwenye serikali ya kikoloni.

Fernando Peyroteo alianza kupambania ndoto yake ya kuwa mwanamichezo kwa kushiriki michezo tofauti tofauti ambapo inatajwa aliwahi kujaribu michezo takribani 9 ndipo alikuja kuibukia kwenye mchezo wa soka.

Mwaka 1937 alijiunga na klabu ya Sporting CP akitokea klabu ya Clube União Fabril), klabu ndogo nchini Ureno ambapo Sporting CP ilivutiwa na kiwango chake akiwa kijana mdogo mwenye umri wa miaka 19 ndipo aliwashangaza wengi kwa wakati huo kwa kuwa moja ya nyota waliyowavutia watu wengi ndani ya taifa la ureno kipindi hicho.

Ndani ya kipindi cha miaka 12 ya kuitumika klabu ya sporting CP alifanikwa kufunga magoli takribani 540 katika mechi 334 ambazo ni rasmi yaliyoweza kuorodheshwa kwenye kumbukumbu ya majarida mbalimbali ila inatajwa ya kuwa aliwahi kufunga mabao mengi Zaidi ya hayo.

Vilevile  amewahi kutwaa mataji kama vile Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ureno (Primeira Divisão) – mara 5, Taji la Kombe la Ureno (Taça de Portugal) – mara 4, Troféu Lisboa na mashindano mengine ya ndani na yale ya klabu bingwa barani ulaya.

Alistaafu soka mwaka 1949, akiwa na umri wa miaka 31, kwa sababu ya majeraha. Baada ya kustaafu, maisha yake yalikuwa magumu kidogo, akijaribu kazi mbalimbali zikiwemo ukocha kwa muda mfupi (aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Ureno kwa kipindi kifupi mwaka 1961, bila mafanikio).

Je nini kilichomfanya Fernando Baptista de Seixas Peyroteo de Vasconcelos kutokuwa maarufu Zaidi duniani?

Nyota Fernando Peryroteo hakuwa maarufu kutokana na kucheza soka katika enzi ambazo soka halikuwa na matangazo ya televisheni ya kimataifa, kamera nyingi uwanjani, wala mitandao ya kijamii  Habari kuhusu wachezaji wa enzi hizo zilibaki ndani ya nchi zao au magazeti ya wakati huo, Hivyo, hata rekodi zake kubwa hazikusambaa duniani.

Vilevile hakuwahi kushiriki kombe la dunia Ureno haikufuzu kwa Kombe lolote la Dunia wakati wa kipindi chake cha kucheza.Hii ilimnyima fursa ya kujitangaza kwa kiwango cha kimataifa kama ambavyo ilivyowatokea Pele, Maradona, au Ronaldo. Aliichezea timu ya taifa ya Ureno mechi 20 tu, na kufunga mabao 14 — idadi ndogo ikilinganishwa na uwezo wake mkubwa.

Pia Hakuwahi kucheza soka nje ya Ureno, kwa mfano kwenye klabu kubwa za Hispania, Italia, Uingereza au Amerika Kusini. Hii ilimfanya abakie kuwa "nyota wa ndani", tofauti na wachezaji waliocheza kimataifa vilevile alistaafu mapema kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kwa nyakati tofauti.

Baada ya kustaafu Fernando Peryroteo hakuishi Maisha kama mtu maarufu ila Alijaribu ukocha mara moja tu akiwa kocha wa timu ya taifa ya Ureno kwa muda mfupi, mwaka 1961, lakini hakufanikiwa.

Hivyo jina la Peyroteo likazama polepole, japo rekodi zake hazikupitwa kwa muda mrefu kama vile asilimia ya kufunga mabao kwa kila mechi ni kubwa ajabu karibu bao 1.6 kwa kila mechi. Alifariki mapema, mwaka 1978, akiwa na umri wa miaka 60, na hakuweza kushuhudia mapinduzi ya kisasa ya vyombo vya habari na kumbukumbu za kihistoria kama walivyofaidika nyota wengine kama Puskás, Di Stéfano, Pelé, Cruyff, na baadaye Maradona.

Ingawa hakupata sifa kubwa kimataifa kwa sababu soka halikuwa limeenea sana ulimwenguni wakati huo, anaenziwa sana na mashabiki wa Sporting CP.


+255617784260


0/Post a Comment/Comments