Na Rashid Msiri
Maisha ya soka yamejaa mengi yenye kushangaza kutokana na mengi yenye kuvutia yanayoacha kumbukumbu nyingi njema zenye kuvutia na kushangaza wengi kwa vizazi na vizazi hali inayopelekea kuwa na wapenzi na mashabiki wengi kwa wa mchezo huo duniani kote.
Kila siku inakadiriwa ya kuwa duniani kote ni zaidi ya mechi 300 hadi 1500 ya mechi za mpira wa miguu huchezwa duniani kote kulingana na ratiba ya michezo ya michuano tofauti tofauti ambayo michuano hiyo huleta mvuto na hamasa yenye kuvutia hali ambayo hupelekea kuzalishwa kwa upinzani mkubwa unaobeba hisia za wengi na ushindani miongoni mwamashabiki wa soka kutokana mchanganyiko wa sababu za kihistoria, kijamii, kijiografia, kisiasa, kiutamaduni, na hata kiuchumi.
Sahau kuhusiana na derby ya kariakoo ambayo imebeba ushindani wa kihistoria kwa zaidi ya miaka 80 ya vilabu vya simba na yanga kutokana na mgawanyiko wa mashabiki wa vilabu hivyo viwili kwa eneo kubwa la Jiji la Dar-es-salaam makazi ya asili ya vilabu hivyo na kusambaa kwa hisia nzuri na ngumu zisizoelezeka miongoni mwamashabiki ni suala la heshima kubwa, ni zaidi ya pointi, ni fahari ya mtaa, klabu na mashabiki.
Kwa kifupi, Derby ya Kariakoo ni zaidi ya mchezo; ni tukio la kijamii, kihistoria, na kiutamaduni linaloonyesha uzito wa soka katika maisha ya Watanzania huku ikileta athari ya moja kwa moja kwa ushawishi wa siasa, biashara, na mazungumzo ya kila siku kwa kipindi chote kabla na baada ya mechi.
Pia huambatana na maandalizi makubwa ya kiutamaduni, kama vile gwaride la mashabiki, mavazi ya timu ambapo hapa hubebwa na utamblisho wa pande zote mbili kwa rangi nyekundu na nyeupe kwa upande wa mashabiki wa simba narangi za kijani na njano kwa mashabiki wa yanga.
Vilevile kukua kwa teknolojia kumeleta athari chanya na kuongeza kampeni za mitandaoni juu ya ubora wa vilabu hivyo viwili kila pale unapokaribia mchezo wa Derby ya Kariakoo.
Huu ni mfano tuuh wa Derby ya kariakoo unavyokusanya historia na hamasa ya jamii ya wa swahili katika mchezo wa soka na eneo kubwa la kusini mwa jangwa la sahara.
Kwa zaidi ya maili 4500 kutokea jijini Dar-es-salaam tunaipata derby nyingine inaoyeleza juu ya hisia za kweli za kupendwa kwa mchezo wa mpira wa miguu,
Ni El Clásico hii ni derby inayowakutanisha Real madrid na FC Barcelona "El Clásico" ni Kihispania kwa maana ya "Mchezo wa Kihistoria" mchezo huu umebeba rekodi nyingi za kushangaza dunia huku ukishuhudia vipaji vikubwa vikitawala historia na takwimu za mechi kwa vizazi na zizazi kwa kujumisha nyota kama vile Cristiano Ronaldo,Alfredo Di Stéfano,Zinedine Zidane,Raúl González kwa upande wa Realmadrid ila kwa upande wa wapinzani wao FC Barcelona ni nyota kama Lionel Messi,Xavi Hernández,Andrés Iniesta,Ronaldinho na Neymar Jr
Ila unafahamu ya kuwa derby ya El Clásico imebeba rekodi ya kuvutia iliyojifichwa kwenye Alphabet A-Z za lugha ya kiingereza ?
Kwa kuanza na herufi A hii inasimama kama utambulisho wa gwiji wa klabu ya Realmadrid Alfredo Di Stéfano ambaye alitawala El Clásico katika miaka ya 1950–60.Upande wa herufi B hii inasimama kwa upande wa uwanja wa Santiago Bernabéu, unaomilikiwa na klabu ya Real Madrid ya Hispania, umepitia ukarabati mkubwa uliolenga kuuboresha kuwa moja ya viwanja vya kisasa zaidi duniani. Ukarabati huu ulianza mwaka 2019 na unakadiriwa kugharimu zaidi ya €900 milioni ambapo hivi sasa unaingiza mashabiki 85,000 kwa wakati mmoja.
Herufi C imesimama kwa niaba ya gwiji wa soka duniani kwa sasa anayetajwa kuwa ni mchezaji mwenye magoli mengi kwa sasa takribani magoli 1000 Cristiano Ronaldo yeye ndiye Mfungaji mashuhuri wa Real Madrid katika El Clásico mabao 18 katika michezo 30 aliyowahi kuicheza ya derby hiyo.
Herufi D inasimama kwa heshima – Decima (La Décima) ambalo La Décima ni jina lililotolewa kwa ubingwa wa 10 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) kwa klabu ya Real Madrid – taji ambalo walilitafuta kwa miaka mingi baada ya kushinda kwa mara ya 9 mwaka 2002 ndipo baada kutwaa taji la 10 msimu wa UEFA 2013/14 lilizaliwa jina la decima Ingawa ni kuhusu UEFA Champions League, ushindani wa Barca vs Madrid uliathiri safari ya Decima kwa Madrid.
Na herufi inasimama kwa niaba ya E – El ClásicoJina lenyewe la mechi – linamaanisha “mchezo wa kihistoria.” kwa zaidi ya miaka 100 ya ushindani wa vilabu hivi.
Herufi F inasimama kwa niaba ya mchezaji Figo (Luis Figo) Aliyekuwa mchezaji wa Barcelona kisha akaenda Real Madrid hali iyopelekea kuonekana kuwa ni msaliti kwa miongoni mwamashabiki wa Barcelona hali iliyopelekea chuki kubwa juu yake hadi kufikia hatua ya kurushiwa kichwa cha nguruwe katika mchezo mmoja wa el clasico.
Herufi G inasimama kwa niaba ya kocha – Guardiola (Pep Guardiola)Kocha aliyefanya Barcelona kutawala El Clásico kati ya 2008–2012 kwa kuwa mwanzilishi wa falsafa ya mpira ya TikTak iliyoipa heshima kubwa na mvuto wa kiuchezaji wa klabu ya FC Barcelona duniani kote.
Herufi H inasimama kwa upande wa Hat-trick zilizowahi kufungwa katika mchezo wa EL Clasico na wachezaji mbalimbali kama vile Lionel Messi,Romário,Estanislao Basora huku Luis Suárez ndiye mchezaji wa karibu zaidi kufunga hat-trick amefunga mwaka 2018 na kwa upande wa wachezaji wa madrid waliowahi kufunga hat-trick ni Iván Zamorano na gwiji Ferenc Puskás, Messi aliwahi kufunga hat-trick ya kihistoria dhidi ya Madrid mwaka 2007.
Herufi I inasimama kwa niaba ya jina la Andres Iniesta Kiungo wa Barcelona aliyejulikana kwa utulivu na ubunifu kwenye mechi za El Clásico hali iliyopelekea kuwahi kupongezwa kwa kupigiwa makofi na mashabiki wa Realmadrid katika moja ya mechi za el clasico.
Herufi J inasimama kwa niaba ya kocha José Mourinho ambaye aliwahi kuwa Kocha wa Real Madrid aliyeingiza "moto wa vita" kwenye El Clásico miaka ya 2010–2013.
Herufi K inasimama kwa upande Kadi (Red & Yellow Cards) mechi hii imekuwa na kadi nyingi zaidi kuliko mechi nyingi kubwa barani Ulaya.
Herufi L inasimama kwa niaba ya mchezaji nyota – Lionel Messi mfungaji bora wa muda wote wa El Clásico (mabao 26), pia ndiye mchezaji mwenye mataji mengi duniani na ndiye mchezaji mwenye tuzo nyingi za mchezaji bora duniani ya Ballon Dor akiwa na tuzo 8.
Herufi M inasimama kwa maana ya neno Manita hili ni neno la Kihispania kwa maaba “kofi la vidole 5” matokeo ya aibu kwa Madrid mwaka 2010
Neymar Jr aliwahi kuwa sehemu ya "MSN" ya Barcelona (Messi, Suárez, Neymar) iliyotisha Madrid nahii inasimama kwa upande wa herufi N.O Inasimama kwa upande wa Own goals (Mabao ya kujifunga) Kuna mechi chache ambazo zimeamuliwa kwa mabao ya kujifunga katika El Clásico.
P inasimama kwa niaba ya mchezaji Piqué (Gerard Piqué) Beki wa Barcelona na mhusika mkuu kwenye mvutano wa kihisia na Real Madrid kutokana nayeye kuwa mzawa halisi wa jimbo la katalunya inakotokea klabu ya Barcelona ambao wanaupinzani mkubwa na serikali ya hispania yenye makao makuu Katika jiji la Madrid wakihitaji kijitenga kuwa nchi huru.
Q inasimama kwa niaba ya magoli ya mapema kuwahi kufungwa katika mchezo huo ,Mara kadhaa El Clásico imekuwa na mabao ya mapema, ndani ya dakika za mwanzo huku mchezji Karim Benzema ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya bao la mapem zaidi kufungwa kwenye El clasico, Sekunde ya 21 (Real Madrid vs Barcelona, 2011)
R inasimama kwa niaba ya Ramos (Sergio Ramos) kaka jambazi ambaye ni beki wa katinwa Realmadrid Alicheza El Clásico nyingi zaidi kwa Real Madrid Pia ndiye mchezaji aliyepewa kadi nyekundu nyingi katika mchezo huo.
S inasimama kwa niaba ya mchezaji Suárez (Luis Suárez) Aliwahi kufunga mabao mengi dhidi ya Madrid, ikiwa ni pamoja na hat-trick mwaka 2018.
T inasimama kwa niaba ya neno Tiki-Taka Mtindo wa Barcelona chini ya Guardiola uliotawala El Clásico ni mtindo wa uchezaji wa mpira wa miguu uliyoitesa Realmadrid kwa kiasi kikubwa.
U inasimama kwa niaba ya Ushindi mkubwa zaidi kuwa kutokea kweye el clasico Real Madrid 11–1 dhidi ya Barcelona (1943 Copa del Rey) ushindi huu wa kihistoria unasimama kama kichapo kikubwa zaidi kuwahi kutokea
V inasimama kwa niaba ya nyota wa realmadrid VinÃcius Jr Nyota wa Real Madrid, anayetabiriwa kuwa tishio jipya katika El Clásico kwa muda mrefu kutokana na kipaji chacke kikubwa ndani ya klabu hiyo.
Herufi W inasimama kwa Wins (Ushindi)
El Clásico imekuwa na ushindani mkubwa sana – mara nyingi Barcelona na Madrid hufuatana kwa ushindi karibu sawa
Herufi X inasimama kwa niaba ya nguli wa FC barcelona Xavi Hernández Aliyekuwa kiungo bora wa Barcelona na sasa kocha, aliyehusika katika mechi nyingi za El Clásico.
Herufi Y inasimama kwa upande wa Yellow Cards (Kadi za Njano) Mechi za El Clásico hujaa hisia kali, na hivyo mara nyingi huwa na kadi nyingi za njano.
Herufi Z inasimama kwa niaba Zidane (Zinedine Zidane) Mchezaji na kocha wa Real Madrid aliyeheshimika sana, aliyeshinda El Clásico kadhaa kama mchezaji na kocha wa timu hiyo bila ya kusahau rekodi yake ya kuvutia katika michuano ya klabu bingwa ulaya kutwaa taji hilo mara tatu mtawalia.
Hii yote inakuonesha juu ya upinzani na utamu wa mchezo wa mpira wa miguu duniani hali inayopelekea kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi ndani mchezo huo wa soka El clasico ni moja tuu ya derby zinazoweza kuwa alama ya ladha halisi ya mchezo wa Soka.
rashidmsiri@gmail.com
0744699171
Post a Comment