Klabu ya Chelsea imeweka rekodi ya aina yake barani Ulaya baada ya kuichapa Real Betis ya Hispania kwa mabao 4-1 katika fainali ya UEFA Conference League iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Stadion Miejski, nchini Poland. Ushindi huo umeifanya Chelsea kuwa timu ya kwanza barani Ulaya kutwaa vikombe vyote vikuu vya mashindano ya bara hilo.
Katika mchezo huo, Real Betis walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 9 kupitia kwa Abdesamad Ezzalzouli. Chelsea ilisawazisha dakika ya 65 kupitia Enzo Fernández, kabla ya Nicolas Jackson kufunga bao la pili dakika ya 70. Bao la tatu liliwekwa kimiani na Jadon Sancho dakika ya 83, huku Moisés Caicedo akifunga bao la mwisho dakika ya 90 na kuhitimisha ushindi mnono kwa Chelsea.
Kwa ushindi huo, Chelsea sasa imekamilisha makusanyo ya vikombe vyote vya ngazi ya juu barani Ulaya. Hii ni baada ya kutwaa ubingwa wa Conference League kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Vikombe Vilivyotwaliwa na Chelsea hadi Sasa:
-
Ubingwa wa Ligi Kuu ya England (Premier League) – mara 6
-
FA Cup – mara 8
-
Carabao Cup – mara 5
-
UEFA Champions League – mara 2
-
UEFA Europa League – mara 2
-
UEFA Super Cup – mara 2
-
FIFA Club World Cup – mara 1
-
UEFA Conference League – mara 1
Rekodi hii ya kipekee imeifanya Chelsea kuwa klabu ya kwanza barani Ulaya kutwaa makombe yote makuu ya mashindano ya klabu yanayoandaliwa na UEFA pamoja na FIFA
Post a Comment