Na Timothy Lugembe,
Mwanakwetu sports,.
Mchezaji wa Azam FC vijana chini ya umri wa miaka 20 Carlos Chasambi ambaye ni ndugu wa mchezaji wa Simba sc Ladack CHASAMBI ameibuka shujaa katika mchezo wa fainali ya NBC youth league 2024/2025 baada kuifungia Timu yake bao pekee lililo ipa ubingwa dhidi ya vijana wa Fountain gate.
Azam FC ndio mabingwa wapya msimu 2024/2025 huku nafasi ya pili ikishiliwa na Fountain gate , huku washindi wa tatu wakiwa Kagera sugar na mshindi wa nne akiwa ni ken gold pia ikiwa ndio Timu yenye nidham kwenye mashindano hayo, lakini tuzo ya kipa bora ikienda kwa Antony Remmy kutoka Azam FC huku Simba na yanga wakishindwa kuambulia chochote msimu huu baada kuondoshwa hatua za awali kabisa.
Makocha wa Timu zote mbili wazungumzia mchezo na hali ya mashindano kwa ujumla huku kwa upande wa kocha wa Fountain gate Abubakary Ally akisifu mashindano kuwa yalikuwa ni mazuri yenye lengo la kuibua vipaji vya vijana na ushindani ulikuwa mkubwa ila ameahidi msimu ujao watajiandaa na kufanya vizuri.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Azam FC vijana Kassim Liogope amesema mashindano yalikuwa na ushindani hasa kuanzia hatua ya nane Bora ambapo Timu zilikuwa zikizidi kubadilika mchezo Hadi mchezo na kipekee kawapongeza vijana wake kwa kutwaa taji Hilo.
Ligi ya NBC Youth League ni mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini wao, NBC. inaonekana kuwa ni sehemu ya juhudi za TFF kukuza vipaji vya vijana nchini kupitia mashindano ya umri mdogo kama ilivyoainishwa kwenye kanuni za ligi zao
Post a Comment