Yanga inasubiri dakika 90 tu kutinga Fainali


 YANGA sasa inasubiri dakika 90 tu za mchezo wa duru ya pili, nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Marumo Gallants itakayopigwa uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg kuanzia saa 1:00 usiku za Tanzania sawa na saa 12:00 jioni hapa Afrika Kusini.

Tayari Wananchi wamemaliza mipango yote ya kiutawala na muda mchache uliopita wachezaji na benchi la ufundi walikula chakula kisha kufanya kikao cha mwisho kwaajili ya mechi hiyo.

Pia katika mambo ya usafiri, tayari basi maalumu litakalowabeba wachezaji wa Yanga limewasili ambalo limeandaliwa na timu  hiyo, ikiwa ni tofauti na lile walilopewa na wenyeji wao Marumo.

Viongozi, wadau na mashabiki kadhaa wa timu hiyo wanaendelea kufika katika kambi ya Yanga hapa Rustenburg kwaajili ya msafara wa kwenda uwanjani hapo baadae.

Ikumbukwe Yanga  inahitaji ushindi au sare ya aina yeyote katika mchezo wa leo ili kutinga fainali baada ya kushinda 2-0, kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Mei 10, mwaka huu, uwanja wa Benjamin Mkapa, Tanzania.

 

 

0/Post a Comment/Comments