Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kila mchezaji ana eneo ambalo ndilo msingi wa ubora wake katika upachikaji wa mabao, Mwingine anauwezo mkubwa wa kutumia mguu wa kulia, mwingine wa kushoto, huku wengine wakitumia vichwa vyao. Hata hivyo, kwa Cristiano Ronaldo, mambo ni tofauti kwani amekuwa na uwezo wa kufunga kwa kutumia maeneo yote hayo.
Licha ya idadi ya mabao aliyofunga katika maisha yake ya soka, kuna jambo jingine linalomtofautisha na wachezaji wengi ambalo ni uwezo wa kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja kwa kutumia mguu wa kulia, mguu wa kushoto na kichwa, maarufu kama Perfect Hat-trick.
Tangu aanze kucheza soka la ushindani, nyota huyo amefikisha jumla ya Perfect Hat-trick 11, rekodi inayomweka miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa katika eneo hilo.
Kuonyesha kuwa jambo hilo si rahisi wala la kawaida, Lionel Messi, ambaye amekuwa akilinganishwa na Ronaldo katika ubora wa soka duniani, hajawahi kufunga Perfect Hat-trick katika maisha yake ya soka.
Hivyo, kufikisha Perfect Hat-trick 11 kunaonyesha uwezo wa Ronaldo wa kutumia miguu yote miwili na kichwa katika upachikaji wa mabao, jambo linalomtofautisha katika sanaa ya kufunga.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment