Mnyama katanguliza mguu mmoja hatua ya makundi CAFCL


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imepata nafasi ya kucheza michezo yote miwili ya hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya FC 15 de Agosto ya Equatorial Guinea katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hatua hiyo imethibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) baada ya timu zote mbili kushindwa kufikia makubaliano ya kucheza mchezo mmoja nchini Equatorial Guinea na mwingine Tanzania.

Kwa mujibu wa ratiba, FC 15 de Agosto itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza utakaochezwa Oktoba 20, 2026, saa 10:00 jioni, huku Simba SC ikiwa mwenyeji wa mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 25, 2026, saa 10:00 jioni, katika Uwanja wa Uhuru.


Hali hiyo inaipa Simba faida ya kiushindani kutokana na kucheza michezo yote miwili katika uwanja wake wa nyumbani, mbele ya mashabiki wake ambao wanaweza kuipa nguvu timu hiyo katika harakati za kutafuta ushindi na tiketi ya kusonga mbele.

Hata hivyo, licha ya faida ya uwanja wa nyumbani, Simba italazimika kutumia vizuri nafasi zitakazopatikana na kupata matokeo mazuri katika michezo yote miwili, kwani kucheza nyumbani pekee hakutoi dhamana ya kufuzu hatua inayofuata.

Simba sasa ina nafasi ya kutumia uzoefu wake katika mashindano ya Afrika pamoja na sapoti ya mashabiki wake kuweka msingi wa kusonga mbele katika michuano hiyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments