CAF yaweka hadharani tarehe ya michezo hatua ya makundi

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka  barani Afrika (CAF) limetangaza ratiba ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2026/27, huku teknolojia ya usaidizi wa mwamuzi wa video (VAR) ikitarajiwa kutumika katika hatua hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, michezo ya hatua ya makundi itachezwa katika raundi sita kuanzia Novemba 27, 2026 hadi Januari 24, 2027.

Ratiba ya michezo hiyo imepangwa kama ifuatavyo:

- Raundi ya kwanza: Novemba 27–29, 2026.

-Raundi ya pili: Desemba 4–6, 2026.

- Raundi ya tatu: Desemba 18–20, 2026.

-Raundi ya nne: Januari 8–10, 2027.

- Raundi ya tano: Januari 15–17, 2027.

- Raundi ya sita: Januari 22–24, 2027.

Katika hatua nyingine, CAF imetangaza kuwa VAR itatumika katika hatua ya makundi ya mashindano yote mawili, ikiwa ni sehemu ya matumizi ya teknolojia kusaidia waamuzi kufanya maamuzi katika matukio muhimu ya michezo.

Ratiba hiyo inazipa klabu zitakazofuzu hatua ya makundi nafasi ya kupanga maandalizi yao kuelekea mashindano hayo ya ngazi ya klabu barani Afrika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments