Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Brazil imeaga mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Norway katika mchezo wa hatua ya 16 bora, matokeo yaliyoambatana na taarifa ya Neymar kuhitimisha safari yake ya soka katika timu ya taifa.
Alieongoza safari ya Neymar kustaafu soka ni mshambuliaji wa Norway Erling Halaand baada ya kupachika mabao mawili yaliyotoa ushindi kwa timu yake na kufuzu robo fainali ambapo watacheza na England, huku matokeo hayo yakimfanya Neymar kutundika daruga akiwa na umri wa miaka 34.
Neymar, anastaafu soka akiwa amefunga bao mchezo wake wa mwisho na kufikisha mabao 80 yanayomfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu ya taifa ya Brazil.
"Nilijaribu na kujaribu, ilianzia hapa uwanja wa MetLife na sasa nimemaliza hapa , ni mwisho sasa" amesema Neymar kauli inayoelezea kustaafu kwake soka la kimataifa.
Kuondoka kwa Brazil kunahitimisha pia ukurasa wa mmoja wa wachezaji waliobeba sura ya timu hiyo kwa miaka kadhaa, huku Norway ikiendelea na mashindano ikiwa na tiketi ya robo fainali mikononi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com




Post a Comment