Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kwa miaka 10 tangu aanze kuinoa Manchester City mwaka 2016, kocha Pep Guardiola ameifikisha klabu hiyo kwenye jumla ya makombe 20 baada ya kuongeza taji la FA Cup kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Mei 16, 2026 kwenye dimba la Wembley.
Taji hilo limekuwa la pili kwa City msimu huu baada ya awali kutwaa Carabao Cup kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal.
Katika kipindi chake cha miaka 10 ndani ya Manchester City, Guardiola ametwaa mataji sita ya Ligi Kuu England, matano ya Carabao Cup, matatu ya FA Cup, matatu ya Community Shield, taji moja la UEFA Champions League, UEFA Super Cup moja pamoja na Kombe la Dunia la vilabu.
Mafanikio hayo yanaendelea kuongeza rekodi ya Guardiola akiwa mmoja wa makocha walioleta mataji mengi ndani ya Manchester City katika kipindi cha karibuni huku ikioneka ni nyakati za mwisho kwa kocha huyo klabuni hapo mara baada ya kuwepo na tetesi nyingi zinazo muhusisha kuondoka klabuni hapo.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment