Ubingwa EPL Hatihati, Unaweza Kuamuliwa kwa Tofauti ya Magoli

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mbio za ubingwa wa Premier League zimeingia katika hatua ya kusisimua zaidi kufuatia matokeo ya leo ambapo Arsenal imepoteza kwa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya AFC Bournemouth, na hivyo kuongeza presha kubwa katika vita ya kuwani taji.

Kipigo hicho kinaifanya Arsenal kubaki kileleni ikiwa imeacha pengo la alama sita dhidi ya Manchester City wanaowafuatia kwa karibu katika nafasi ya pili, Hata hivyo, City wana faida ya kuwa na michezo miwili mkononi (viporo), hali inayoweza kubadilisha kabisa msimamo wa ligi.

Katika hesabu za ubingwa, iwapo Manchester City watafanikiwa kushinda michezo yao yote miwili ya viporo ukiwemo mchezo mngumu dhidi ya Arsenal basi timu hizo mbili zitafungana kwa alama ,hii inaweka wazi uwezekano mkubwa wa ubingwa kuamuliwa kwa tofauti ya mabao (goal difference), jambo ambalo ni nadra lakini linaongeza msisimko mkubwa katika mbio za ubingwa.

Hii utatokea iwapo city itashinda michezo yake yote kuanzia sasa huku arsenal akipoteza dhidi ya City watafungana alama , na iwapo Kila timu ikishinda michezo yake iliyosalia bas wote kwa pamoja watakuwa wamejikusanyia Jumla ya alama 85 kitakacho amua nani awe bingwa itakuwa ni magoli ya kufunga na kufungwa.

Hata hivyo, matokeo yanaweza kutokea vinginevyo lakini kwa ukubwa mchezo wa April 19,2026 utakao wakutanisha miamba hao kwa kiasi kikubwa ndio utazidi kutoa taswira ya ubingwa kwa upana zaidi

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments