Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Taifa ya DR Congo inatarajiwa kushuka dimbani majira ya saa sita usiku April 1, 2026, katika mchezo muhimu wa kusaka nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Jamaica
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Akron Stadium uliopo nchini Mexico, huku macho ya mashabiki wengi yakielekezwa kuona kama DR Congo wataweza kuandika historia mpya katika historia ya soka lao na Afrika kwa ujumla.
Iwapo DR Congo watafanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo, watakuwa wamekata tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia, hatua ambayo itawawezesha kuungana na mataifa mengine ya Afrika tisa yatakayoshiriki michuano hiyo mikubwa duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment