RATIBA NBC HADHARANI, SIMBA NA YANGA KUUMANA DISEMBA 13

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) imetoa rasmi ratiba ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26, ratiba ambayo imepokelewa kwa vizuri na mashabiki wa soka nchini, Kupangwa kwa ratiba hii kumetoa mwanga mpya wa ushindani unaotarajiwa msimu huu, huku timu 16 zikijiandaa kupambana vikali kuhakikisha zinafanya vizuri.

Ratiba hiyo imeonesha mfululizo wa michezo kuanzia septemba 17, 2025 hadi mei 23, 2026. Wadau wa soka na mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona lini watani wa jadi, Simba SC na Yanga watakutana katika mechi ya Kariakoo Derby mchezo ambao kila mara huvuta hisia kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa ratiba pambano hilo la dabi ya Kariakoo limepangwa kupigwa Disemba 13, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku mchezo wa pili marejeano utafanyika Aprili 4, 2025.

Bodi ya Ligi imetoa wito kwa mashabiki, wadau na klabu zote kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu kwa msimu huu mpya ambao unatarajiwa kuwa na msisimko wa kipekee kutokana na ubora wa timu, maandalizi ya vilabu, na ushindani wa wachezaji wa ndani na wa kimataifa waliopo kwenye ligi.

Kwa mujibu wa TPLB, ratiba hii inaweza kubadilishwa endapo kutakuwa na sababu za kimsingi kama ratiba za kimataifa au mashindano ya CAF zitaingiliana na ratiba ya ligi kuu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments